Katika kuadhimisha Wiki ya LPG 2026, TZLPGA ilishiriki katika kipindi maalumu kilichorushwa kupitia ITV Tanzania, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayoikabili sekta ya LPG nchini.

Kipindi hicho kiliwakutanisha wadau muhimu wa sekta, wakiwemo watumiaji wa LPG kwa matumizi ya taasisi pamoja na Wakala wa Vipimo (WMA), kujadili masuala ya usalama wa matumizi ya LPG, uzingatiaji wa kanuni na taratibu, usahihi wa vipimo na uzito wa mitungi, ulinzi wa mlaji, matumizi mengine ya LPG, n.k.

Majadiliano haya yalitoa fursa muhimu kwa wadau kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto zilizopo na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi, taasisi za serikali na watumiaji wa LPG.

Tunapoendelea kutekeleza ajenda ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, ushirikiano wa wadau wote ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa LPG iliyo salama, ya uhakika, nafuu na endelevu kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *